Friday, 10 June 2016

Maafisa 302 wa polisi waachishwa kazi pwani

















Mwenyekiti wa Tume ya Huduma kwa Polisi nchini NPSC Johnston Kavuludi akiwahutubia wanahabari hapo awali. Alisema kuwa maafisa hao walikiuka sheria za nchini kwa mujibu wa katiba, na ni wazi kuwa walikuwa wakienda kinyume na utendekazi wao.


Maafisa wa trafiki kutoka eneo la Pwani waliokataa kukaguliwa na Tume ya Huduma kwa Polisi nchini NPSC, wameachishwa kazi.

Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na tume hiyo siku ya Alhamisi, maafisa 302 walikwepa ukaguzi ambao ulikuwa ukiendeshwa na Tume ya NPSC mjini Mombasa katika kipindi cha majuma mawili kutathmini utendakazi na maadali ya maafisa hao.

Tume hiyo inayoongozwa na Johnson Kavulundi imesema kuwa imebaini maafisa hao wanakiuka sheria za nchini kwa mujibu wa katiba, na ni wazi kuwa walikuwa wakienda kinyume na utendekazi wao.

“Kukwepa kwa maafisa hao kupigwa msasa kunaashiria kukithiri kwa kashfa za ufisadi nchini zinazowazonga maafisa wengi wa polisi,” alisema Kavuludi.

Inspekta mkuu Jenerali wa Polisi nchini Joseph Boinnet anatarajiwa kuwatumia maafisa hao barua za kuwaondoa kazini.

No comments:

Post a Comment