Sunday, 5 June 2016

Mboko kuwania kiti cha ubunge Likoni


Mwakilishi wa wanawake katika Kaunti ya Mombasa Bi Mishi Mboko ametangaza azma yake ya kuwania kiti cha ubunge cha Likoni katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza alipohudhuria mashindano ya soka ya wanadada katika uwanja wa Mombasa Sports Club siku ya Jumatano, Mboko alisema tayari amefanya maamuzi na kuwa hakuna kitakachomzuia kukinyakua kiti hicho.
‘’Nasema na naapa nitakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Mombasa kuchaguliwa mbunge. Hicho kiti cha ubunge wa Likoni nitachukua katika uchaguzi wa 2017,” alisema Mboko.
Aidha, Bi Mboko ametoa wito kwa akina mama katika ukanda wa Pwani kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao badala ya kusubiri kutengewa viti maalum.
‘’Akina mama nasi pia tuna uwezo tu kama walionao wanaume. Tujitose kwenye kinyanganyiro sauti zetu tuzidhihirishe,” aliongeza Mboko.
Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Mombasa Mishi Mboko katika hafla ya awali.

No comments:

Post a Comment