Nimesimama kidete, kumsifu muungwana
Sio jakaya kikwete, nisikizeni kwa kina
Jicho pevu mumuite, nyali anapambana
Kiongozi wa ukweli, wa busara na heshima
Sio jakaya kikwete, nisikizeni kwa kina
Jicho pevu mumuite, nyali anapambana
Kiongozi wa ukweli, wa busara na heshima
Wa busara na heshima, asiekuwa tapeli
Kwa haki amesimama, tushaziona dalili
Kasaidia kina mama, na kujali zao hali
Kiongozi wa ukweli, kwa jina Mohamed Ali
Kwa haki amesimama, tushaziona dalili
Kasaidia kina mama, na kujali zao hali
Kiongozi wa ukweli, kwa jina Mohamed Ali
Kwa jina Mohamed Ali, kila pembe anavuma
Tuungane wa nyali, tumpeni wa hikima
Tusidanganywe na mali, tukaumiza mtima
Kiongozi wa kweli, ndie huyu jicho pevu
Tuungane wa nyali, tumpeni wa hikima
Tusidanganywe na mali, tukaumiza mtima
Kiongozi wa kweli, ndie huyu jicho pevu
Ndie huyu jicho pevu, mpekuzi wa habari
Kijana aloshupavu, atakae leta mazuri
Ataziponya zetu kovu, kimaisha tunawiri
Kiongozi wa ukweli, kura zetu tumpeni
Kijana aloshupavu, atakae leta mazuri
Ataziponya zetu kovu, kimaisha tunawiri
Kiongozi wa ukweli, kura zetu tumpeni
Kura zetu tumpeni, vijana na kina baba
Hata walimu shuleni, atatimiza mikataba
Nyali tuamkeni, tusijefanywa mazoba
Kiongozi wa ukweli, elfu mbili kumi na saba
Hata walimu shuleni, atatimiza mikataba
Nyali tuamkeni, tusijefanywa mazoba
Kiongozi wa ukweli, elfu mbili kumi na saba
Elfu mbili kumi na saba, ikaribu mewadia
Aifungashe mikoba, huyo alokalia
Amuache aloshiba, aje kutuhudumia
Kiongozi wa ukweli, kura zetu tumpeni
Aifungashe mikoba, huyo alokalia
Amuache aloshiba, aje kutuhudumia
Kiongozi wa ukweli, kura zetu tumpeni
Kura zetu tumpeni, kwa yake njema kauli
Huyu mpenda amani, na maendeleo ya kweli
Sipompa tajutani, yawe yale ya awali
Jicho pevu tumpeni, eneo bunge la nyali
Huyu mpenda amani, na maendeleo ya kweli
Sipompa tajutani, yawe yale ya awali
Jicho pevu tumpeni, eneo bunge la nyali
By MentalSickmind #DWAH_DWAH
No comments:
Post a Comment